Saturday, August 4, 2012

MAHARAMIA WASHAMBULIA MELI ZA MAFUTA NCHINI NIGERIA


Watu wenye silaha wameshambulia meli mbili nje ya eneo la mafuta la Nigeria, eneo la mdomo wa Mto Niger.
 
Walinzi wawili waliuwawa na wawili kujeruhiwa katika shambulizi hilo.

Washambuliaji hao, ambao hawakujulikana, pia waliwateka nyara mabaharia wanne.

Jeshi la wanamaji la Nigeria nalo linashiriki kuwasaka washambuliaji hao.

Shambulio hilo limetokea siku tu baada ya serikali ya Nigeria kutangaza kuwa itatumia satalaiti kuzuwia magendo ya mafuta katika eneo hilo, ambayo huuzwa kwenye soko la kimataifa. 
 

SUDAN NA SUDAN KUSINI SASA WAPATANA



Mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki, ametangaza mapatano baina ya Sudan na Sdudan Kusini kuhusu malipo ya mapato ya mafuta baada ya mzozo wa miezi kadhaa, ambao ulikaribia kuingiza mataifa hayo mawili vitani.

Bwana Mbeki aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kwamba maswala yote yaliyokuwa yamebaki, sasa yametatuliwa, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Sudan na jirani yake hajakusema kitu hadi sasa.

Sudan Kusini ilisitisha usafirishaji wa mafuta kupitia Sudan mwezi wa Januari, kufuatia mzozo kuhusu ada iliyokuwa ikitozwa na serikali ya Khartoum. 

BBC SWAHILI

Saturday, July 28, 2012

MAZUNGUMZO YA SUDAN YAKWAMA TENA

Wapiganaji wa SPLM-North 
Wapiganaji wa Sudan wanasema kuwa mazungumzo na serikali ya Sudan kuhusu shida za watu karibu na mpaka wa Sudan Kusini, yamevunjika. 

Akizungumza na BBC, Yasir Arman wa chama cha SPLM North, ameishutumu serikali ya Sudan, kuwa inajaribu kuzusha maswala ya siasa kwenye mazungumzo, na wakati wake haukufika, alisema.

Bwana Arman alisema watu 1,000 wanavuka kila siku kutoka Blue Nile na Kordofan Kusini, na kuingia Sudan Kusini, ili kukimbia njaa na magonjwa - na hivo kuleta maswala ya siasa kwa sasa ni kutoa mazungumzo kwenye mkondo unaofaa.

Watu wengi wamekimbia mapigano, na hivo kuacha kilimo na kufanya watu wengi kukosa chakula. 
 

Friday, July 27, 2012

UHOLANZI YASITISHA MSAADA KWA RWANDA

Serikali ya Uholanzi imesitisha msaada wa dola milioni 6.15 kwa Rwanda baada ya nchi hiyo kuhusishwa na udadhili wa waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hatua hii inajiri siku kadhaa baada ya Marekani kutangza inanuia kupunguza msaada wa kijeshi kwa Rwanda.

 
Hata hivyo Rwanda imekuwa ikikanusha madai ya umoja wa mataifa kuwa inafadhili kundi la waasi wa M23 mashariki mwa DR Congo. 
Waasi hao walianza kutoka jeshini kuanzia mwezi Aprili na hadi kufikia sasa takriban watu 200,000 wametoroka makwao kwa sababu ya mapigano kati ya jeshi na waasi hao.

Hatua hii ya Udachi inajiri baada ya afisaa mkuu wa umoja wa mataifa kuambia BBC kuwa wanajeshi wanaotoka katika jeshi la DRC wamekiri kusajiliwa na Rwanda.

Mnamo siku ya Alhamisi, Umoja wa mataifa uliripoti kuwa wanajeshi wake walisaidia jeshi la DRC kuwafukuza waasi hao kutoka mji wa Goma kwa kutumia helikopta pamoja na magari ya kijeshi.


Mfumo wa sheria

Mwandishi wa BBC mjii Hague, Anna Holigan, anasema kuwa hii ndio hatia ya kwanza ya kifedha kuwa rais Kagame huenda ameanza kuwapoteza washirika wake wa Ulaya.

Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi, amethibitisha kuwa kuanzia sasa haitafadhili vyovyote serikali ya Rwanda hadi pale itakapoweza kuhakikishiwa na Rwanda kuhusiana na madai hayo.

Pesa hizo ilizokuwa inapokea Rwanda zilikuwa zinatumika kuinia hadhi ya mfumo wa sheria wa Rwanda, ingawa mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea kufadhiliwa.

Serikali ya Udachi hata hivyo ingali inasubiri jibu kutoka kwa Rwanda kuhusiana na hatua hiyo wakati ikiendelea kushauriana na nchi zingine za Ulaya kuhusu hatua zaidi dhidi ya Rwanda.


BBC SWAHILI

Thursday, July 26, 2012

KABURU ALIYEPANGA NJAMA ZA KUMUUA MANDELA AKUTWA NA HATIA

Mike du Toit ana hatia ya kutaka kumuua Mandela
Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.

Mahakama ya Pretoria ilimpata kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora alipatikana na hatia ya kupanga kummua Mandela mwaka 2002.
Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.

Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 Afrika kusini.

Wachanganuzi wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana katiki ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.

Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.

Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.

UINGEREZA YATHIBITISHA KUWA NA KIKOSI MAALUM SOMALIA

Mwanajeshi wa Uganda ni mmoja wa wanajeshi wa AMISOM
Serikali ya Uingereza kwa mara ya kwanza imethibitisha kuwa ina kikosi maalum cha jeshi ndani ya Somalia. 

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kwamba katika makao makuu wa jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia kuna washauri 10 wa kijeshi toka Uingereza.
Jeshi hilo la Umoja wa Afrika limekuwa ndani ya Somalia likipambana na wapiganaji wa Al shabaab ambao wanadhibiti maeneo mengi nchini Somalia lakini mwandishi wa BBC amesema kuwa baadhi ya maafisa hao wanaosemekana kuwa ni washauri wameonekana maeneo ya Afgoye ambao hivi majuzi ulutekwa kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab.

Kundi la al-Shabab ambalo mapema mwaka huu lilijiunga na al-Qaeda linadhibiti maeneo mengi nchi Somalia. Mengi ya maeneo hayo yako Kusini na katikati mwa Somalia.
Hata hivuo Al shabaab kwa wakati huu wamebanwa kutoka pande zote.

BBC SWAHILI

RAIS KAGAME ATISHIWA KUSHITAKIWA ICC

Afisa mmoja wa ngazi ya juu nchini Marekani ameonya kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, huenda akafunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita kwa kuhusika na vita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Stephen Rapp, ambae ni mkuu wa kitengo cha jinai ya kimataifa nchini Marekani, amesema hii inatokana na madai kuwa Rwanda inawafadhili waasi wanaopigana katika mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Afisa huyo amesema kuwa Rais Kagame huenda akashtakiwa katika mahakama ya jinai ya kimataifa katika The Hague kwa madai ya kuwafadhili waasi.

Ripoti ya hivi majuzi ya Umoja wa mataifa juu ya mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Congo iliituhumu Rwanda kwa kuyawapa silaha makundi ya waasi.

Hata hivyo Rais Paul Kagame mwenyew amekanusha mara kadhaa kwamba serikali yake ina husika kivyovyote na hita hivyo vya Congo.

Kagame amepuuza habari hizi akisema kwamba maoni yao hayakujumuishwa na walioandika ripoti hizo za kuwalaumu.

HUKUMU YA CHARLES TAYLER LEO

Majaji katika mahakama maalum kuhusu vita nchini Sierra Leone, leo watatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu miaka 10.
Charles Taylor
Taylor anasema kesi hiyo ni njama ya kisiasa

Ikiwa atapatikana na hatia atakuwa rais mstaafu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa.

Kiongozi huyo wa zamani anadaiwa kufadhili waasi wa RUF anakabiliwa na mashitaka 11 yakiwemo ya ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone.

Zaidi ya mashaidi 100 wamefika mbele ya mahakama hiyo lakini Bw Taylor amekanusha kuhusika na uhalifu huo wakivita na anadai kuwa kesi hiyo ni njama ya kummaliza kisiasa.
Hukumu ya majaji hao inasubiriwa kwa hamu sana na raia nchini Sierra Leone ambao jamaa zao waliathirika sana wakati wa vita hivyo.

Inakadiriwa kuwa zaidi wa watu elfu 50 waliuawa na wengine wakiwemo wanawake na watoto walibakwa na kukatwa mikono au miguu na waasi wa RUF ambao upande wa mashtaka unasema walipata usaidizi wa silaha kutoka kwa Bw Taylor.

Wakati wa vita hivyo, mwendesha mashtaka anasema kuwa Taylor alikuwa kiungo muhimu katika biashara haramu ya almasi kutoka Sierra Leone.

Kesi hii iliodumu miaka mitatu na nusu, hata hivyo huenda isi kamilike leo kwani pande zote wanauhuru wa kukata rufaa ikiwa hukumu hiyo haitawaridhisha.

BBC SWAHILI

Saturday, July 21, 2012

VITENDO VYA UKATILI VYAONGEZEKA MAGHARIBI MWA IVORY COAST

Idadi ya watu waliouawa katika vitendo vya ukatili vilivyotokea katika mji wa Duekoue magharibi mwa Ivory Coast imeongezeka.

Habari zinasema kuwa, mapigano makali yamezuka katika kambi ya wakimbizi katika eneo la Nahibly karibu na mji wa Duekoue na kusababisha vifo vya watu 11.

Mapigano ya mara kwa mara ya kikabila huko magharibi mwa Ivory Coast yamesababisha ukosefu wa usalama katika maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo. Watu 3000 wengi wao wakitoka katika mji huo wa Duekoue waliuawa nchini Ivory Coast katika machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

DRC YAVITAKA VIKOSI VYA UMOJA WA MATAIFA VIENDELEE KUWEPO MASHARIKI MWA NCHI HIYO

Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamevitaka vikosi vya majeshi ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuwepo mashariki mwa nchi hiyo kwa ajili ya kupambana na waasi wa M23.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo hivi karibuni alitangaza kusikitishwa kwake na hali inayoendelea katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo na kusema kuwa inatia wasiwasi. Wiki iliyopita pia msemaji wa vikosi vya UN nchini Congo alizungumzia hali ya eneo la mashariki mwa Congo na kusema kuwa, waasi wa Mai Mai wanadhibiti mji wa Walikale.

Duru za habari zinasema kuwa, kufuatia kushadidi kwa mapigano yanayofanywa na waasi hao mamia kadhaa ya askari wa Congo wamelazimika kukimbilia katika maeneo ya askari wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kupata hifadhi.