Mbunge wa Misri wa chama cha
Kiislamu chenye msimamo mkali, amepatikana na makosa ya kuvunja adabu ya
kijamii, kuhusu tukio ambapo amekutwa anafanya mapenzi ndani ya gari
lake.
Kesi hiyo imewatia aibu Waislamu wanaoitwa Salafi - ambao wanadai kuwa wanaume watengwe kabisa na wanawake.
Mbunge huyo, Ali Wanis, alipewa hukumu ya
kifungo cha mwaka mmoja na nusu, kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi, na
kwa kumshambulia askari polisi.
Mbunge huyo ni wa chama cha Nour, kwenye bunge
la mwanzo kuundwa baada ya utawala wa Rais Mubarak - bunge ambalo
lilifutwa mwezi uliopita baada ya mahakama kuamua kuwa bunge hilo siyo
halali.
No comments:
Post a Comment