Thursday, July 26, 2012

HUKUMU YA CHARLES TAYLER LEO

Majaji katika mahakama maalum kuhusu vita nchini Sierra Leone, leo watatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu miaka 10.
Charles Taylor
Taylor anasema kesi hiyo ni njama ya kisiasa

Ikiwa atapatikana na hatia atakuwa rais mstaafu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa.

Kiongozi huyo wa zamani anadaiwa kufadhili waasi wa RUF anakabiliwa na mashitaka 11 yakiwemo ya ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone.

Zaidi ya mashaidi 100 wamefika mbele ya mahakama hiyo lakini Bw Taylor amekanusha kuhusika na uhalifu huo wakivita na anadai kuwa kesi hiyo ni njama ya kummaliza kisiasa.
Hukumu ya majaji hao inasubiriwa kwa hamu sana na raia nchini Sierra Leone ambao jamaa zao waliathirika sana wakati wa vita hivyo.

Inakadiriwa kuwa zaidi wa watu elfu 50 waliuawa na wengine wakiwemo wanawake na watoto walibakwa na kukatwa mikono au miguu na waasi wa RUF ambao upande wa mashtaka unasema walipata usaidizi wa silaha kutoka kwa Bw Taylor.

Wakati wa vita hivyo, mwendesha mashtaka anasema kuwa Taylor alikuwa kiungo muhimu katika biashara haramu ya almasi kutoka Sierra Leone.

Kesi hii iliodumu miaka mitatu na nusu, hata hivyo huenda isi kamilike leo kwani pande zote wanauhuru wa kukata rufaa ikiwa hukumu hiyo haitawaridhisha.

BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment