Saturday, July 21, 2012

MELI YA MAFUTA YALIPUKA NIGERIA

Taarifa kutoka Nigeria zinasema watu kama kumi wamekufa kwenye moto uliotokea kwenye meli iliyobeba mafuta, kwenye bandari ya Port Harcourt.

Matangi ya mafuta nchini Nigeria
Inaarifiwa moto huo ulisababishwa na cheche za moto kutoka ukarabati uliokuwa ukifanywa.

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema baadhi ya watu waliorushwa majini na mripuko huo, walinusurika, lakini wengi wengine walinasa ndani wa meli.

Inadaiwa wazima moto hawakuweza kufikia meli hiyo, kwa sababu mipira ya maji ilikuwa mifupi.

BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment