Saturday, July 21, 2012

VITENDO VYA UKATILI VYAONGEZEKA MAGHARIBI MWA IVORY COAST

Idadi ya watu waliouawa katika vitendo vya ukatili vilivyotokea katika mji wa Duekoue magharibi mwa Ivory Coast imeongezeka.

Habari zinasema kuwa, mapigano makali yamezuka katika kambi ya wakimbizi katika eneo la Nahibly karibu na mji wa Duekoue na kusababisha vifo vya watu 11.

Mapigano ya mara kwa mara ya kikabila huko magharibi mwa Ivory Coast yamesababisha ukosefu wa usalama katika maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo. Watu 3000 wengi wao wakitoka katika mji huo wa Duekoue waliuawa nchini Ivory Coast katika machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

No comments:

Post a Comment