Afisa mmoja wa ngazi ya juu
nchini Marekani ameonya kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, huenda
akafunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita kwa kuhusika na vita katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ripoti ya hivi majuzi ya Umoja wa mataifa juu ya mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Congo iliituhumu Rwanda kwa kuyawapa silaha makundi ya waasi.
Hata hivyo Rais Paul Kagame mwenyew amekanusha mara kadhaa kwamba serikali yake ina husika kivyovyote na hita hivyo vya Congo.
Kagame amepuuza habari hizi akisema kwamba maoni yao hayakujumuishwa na walioandika ripoti hizo za kuwalaumu.
No comments:
Post a Comment