Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamevitaka vikosi vya
majeshi ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuwepo mashariki mwa nchi hiyo kwa
ajili ya kupambana na waasi wa M23.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa
nchini Congo hivi karibuni alitangaza kusikitishwa kwake na hali
inayoendelea katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo na kusema kuwa
inatia wasiwasi. Wiki iliyopita pia msemaji wa vikosi vya UN nchini
Congo alizungumzia hali ya eneo la mashariki mwa Congo na kusema kuwa,
waasi wa Mai Mai wanadhibiti mji wa Walikale.
Duru za habari zinasema kuwa, kufuatia kushadidi kwa mapigano yanayofanywa na waasi hao mamia kadhaa ya askari wa Congo wamelazimika kukimbilia katika maeneo ya askari wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kupata hifadhi.
No comments:
Post a Comment