Taarifa kutoka Marekani
zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani itaipatia Kenya ndege nane
ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kijeshi kwa nchi
za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu
wa Somalia, al-Shabaab.
Moja ya ndege za kijeshi zisizohitaji rubani |
Gazeti la Wall Street Journal la Marekani limearifu kuwa Kenya itapata ndege hizo ambazo hazitakuwa na silaha, lakini zinaweza kugundua maeneo yanayofaa kulengwa na ndege au majeshi ya ardhini.
Gazeti hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani ni sehemu ya msaada wa Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano, na silaha kwa Burundi, Djibouti na Uganda.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment