Sudan Kusini imevunja mazungumzo ya ana kwa ana na
jirani yake, Sudan, yaliyopangwa kufanywa, baada ya kuishutumu Sudan
kuwa imefanya mashambulio mengine ya ndege kwenye ardhi ya Sudan Kusini.
Msemaji wa ujumbe wa Sudan Kusini kwenye
mazungumzo hayo mjini Addis Ababa, Atif Kiir, alisema kwamba mazungumzo
hayo sasa yatafanywa kwa kupitia kamati ya Umoja wa Afrika.
Msemaji wa jeshi la Sudan, alieleza kuwa ndege za jeshi, zililenga wapiganaji waliovuka mpaka na kuingia Sudan.
Umoja wa Mataifa umezipa nchi hizo muda hadi tarehe mbili Agosti, kutatua ugomvi wao kuhusu mpaka na maswala ya usalama.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment