Serikali ya Somalia imetangaza kuwa, imefanikiwa kukamata mtumbwi uliyokuwa umesheheni silaha huko kaskazini mwa nchi hiyo.
Waziri wa Usafirishaji na Kupambana na Uharamia wa Somalia Said Muhammad Raji amesema kuwa, mtumbwi huo unahusishwa na mtandao wa Al Qaeda na ulikuwa umebeba silaha kwa ajili ya wapiganaji wa kundi la as Shabab. Raji ameongeza kuwa, kapteni wa mtumbwi huo alikuwa raia wa Yemen.
Said
Muhammad Raji amesema kuwa, chombo hicho kilikuwa kimebeba mada za
milipuko, guruneti na RPG na kwamba kilikuwa kinaelekea kusini mwa
Somalia.
Wanamgambo wa kundi la as Shabab wanadhibiti baadhi ya maeneo ya kati na kusini mwa nchi hiyo na wanaendelea kupigana na vikosi vya jeshi la serikali ya mpito ya nchi hiyo na vile vya Umoja wa Afrika AMISOM.
No comments:
Post a Comment