Showing posts with label Ajali. Show all posts
Showing posts with label Ajali. Show all posts

Saturday, July 21, 2012

MELI YA MAFUTA YALIPUKA NIGERIA

Taarifa kutoka Nigeria zinasema watu kama kumi wamekufa kwenye moto uliotokea kwenye meli iliyobeba mafuta, kwenye bandari ya Port Harcourt.

Matangi ya mafuta nchini Nigeria
Inaarifiwa moto huo ulisababishwa na cheche za moto kutoka ukarabati uliokuwa ukifanywa.

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema baadhi ya watu waliorushwa majini na mripuko huo, walinusurika, lakini wengi wengine walinasa ndani wa meli.

Inadaiwa wazima moto hawakuweza kufikia meli hiyo, kwa sababu mipira ya maji ilikuwa mifupi.

BBC SWAHILI

Saturday, July 14, 2012

AJALI YA TRENI YAUA WATU 19 AFRIKA KUSINI




Maafisa nchini afrika kusini wanasema takriban watu 19 wameuwawa baada ya treni kugonga lori lililokuwa limebeba wafanyikazi kwenye kivukio cha reli.
Ajali hiyo imetokea katika mkoa wa mashariki wa Mpumalanga.
Habari kamili kuhusu ajali hiyo bado hazijulikani kikamilifu.
Ingawa kuna taarifa nyengine ambazo zinasema kuwa watu wapatao 24 huenda wameuwawa.

BBC SWAHILI